Katika taarifa ya Ofisi ya Ayatollah Sistan, imeelezwa kuwa: Kwa mara nyingine tena jeshi linaloikalia kwa mabavu Palestina limefanya jinai kubwa kwa kuwalenga wakimbizi na waomba hifadhi waliokuwa wanajihifadhi katika Shule ya "Al-Tabeen" katika Ukanda wa Gaza, ambapo jinai hiyo imepelekea kuuawa Kishahidi kwa watu wengi na kujeruhiwa idadi kubwa ya raia wasio na hatia, na jinai hii inaongezwa katika safu ya jinai na uhalifu unaoendelea wa Serikali hii haram na ya kidhalimu, ambayo imekuwa ikiendelea kufanya jinai kwa zaidi ya miezi 10.
Imeelezwa katika taarifa hii kuwa: Katika kipindi cha hivi karibuni, mauaji ya kikhiana imewalenga Viongozi shupavu na mashuhuri wa upinzani (Muqawamah) wanaokabiliana na wavamizi na kuwaua kishahidi. Mauaji ya baadhi yao yamepelekea kukiukwa mamlaka ya nchi kadhaa za eneo, na hali hiyo inaongeza kutokea kwa hatari ya migogoro mikubwa zaidi katika kanda hii (ya Mashariki ya Kati) - Mwenyezi Mungu apishe mbali - Hali hiyo itakuwa na matokeo mabaya kwa nchi na mataifa ya eneo hili.
Taarifa hiyo iliongeza: "Maneno (ibada mbalimbali zinazotolewa) ya kukemea uhalifu huu wa kutisha unaofanywa na wanyama wakubwa wa kibinadamu, ambao hawana maadili na kanuni za juu za kibinadamu hayawezi kusaidia lolote."
Inasikitisha kwamba uungaji mkono usio na kikomo wa idadi ya nchi kubwa Duniani, wanafurahia jinai hizo, na uungaji wao mkono kwa jinai hizo unawazuia kutumia Sheria za Kimataifa kwa wahusika wa uhalifu dhidi ya Ubinadamu.
Mwishoni mwa taarifa hii: Ofisi ya Ayatollah Sistan imeitaka Jumuiya ya Kimataifa kusimama kidete kukabiliana na ukatili huo wa kutisha na kuzuia majeshi ya nchi hiyo kuendelea kutekeleza mipango yao ya kuwadhuru zaidi watu wanaodhulumiwa wa Palestina, na pia kusimamisha mauaji hayo ya kimbari yanayotokana na vita huko Gaza na kuungana kutoa msaada kwa watu wa Gaza.
Imeelezwa katika taarifa hii kuwa: Katika shambulio la mapema asubuhi ya leo (Jumamosi) la utawala ghasibu wa Israel kwenye Shule ya al-Tabeen katika Mji wa Gaza, karibu watu 150 waliuawa Shahidi na makumi ya wengine walijeruhiwa.